Vigezo vyote vya kiuchumi vinaashiria kwamba inchi yenye uchumi mkubwa zaidi barani Afrika ni Nigeria mbele ya Afrika ya kusini iliyokuwa ya kwanza. Leo hii watabiri wa uchumi wanaashiria kuwa inchi hiyo inakaribia kukua kwa kasi kikubwa ifikapo mwaka wa 2050, inakadiriwa kuwa uchumi wake utakuwa kwa viango vya wastani wa 4.2%, ikipanda nafasi nane kutoka 22 hadi 14 chini ya viwango.
Wakati huo huo inaripotiwa kuwa wakati ambao serikali itakuwa imepambana na ufisadi vilivyo, wakaazi wa inchi hiyo wameonyesha tabia ya ujasiriamali ambayo inaendelea kusukuma nchi mbele zaidi.
Itakumbukwa kwamba Nigerian ni moja wapo inchi chache barani afrika Iliyo na uchumi wake mikononi mwao. Yaani uchumi wao haubanui na mataifa ya inje kama wale walio watawala wakati wa ukoloni.
Hio ndio hali ambayo inaonekana katika mataifa mengi yaliyotawaliwa na wafaransa kwa bahati mbaya.
Kulingana na data ya Global Entrepreneurship Monitor, zaidi ya 30% ya wakazi wa Naigeria ni wajasiriamali wapya au wamiliki- kati ya kiwango cha juu zaidi duniani.