Mzozo Kati ya Rwanda na Congo. Kagame amlaumu Tshisekedi kwa ‘kutoheshimu mikataba ya amani’

Rais wa Rwanda Paul Kagame amemshutumu mwenzake wa Congo Felix Tshisekedi kwa kutoheshimu makubaliano kadhaa ya kushughulikia mzozo wa DR Congo.

Mvutano kati ya majirani wa eneo la Maziwa Makuu ya Afrika unaendelea kuongezeka huku DR Congo ikiishutumu Rwanda kwa kuvamia eneo lake “lililojificha kama waasi wa M23”.

Katika hotuba yake kwa mashirika ya kidiplomasia nchini Rwanda Jumatano usiku, Bw Kagame alimkosoa Bw Tshisekedi kwa kushindwa kushughulikia suala la ndani la Congo na kuilaumu Rwanda.

Mamlaka ya Kinshasa haijajibu matamshi ya Bw Kagame.

“Mtu huyu amevunjia heshima mikataba mingi aliyofanya na watu…ikiwa ni pamoja na hata mara ya mwisho mjini Bujumbura”, Bw Kagame alisema. “Tunajadili mambo hadharani, alishiriki, tuliandika taarifa, kuwapa watu yale tuliyojadili na njia ya kusonga mbele.

Taarifa hiyo inasomwa, lakini siku inayofuata taarifa iliyo kinyume inasomwa Kinshasa.” Aliongeza.

Mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika mashariki mwishoni mwa juma lililopita mjini Bujumbura, Burundi, ulielekeza “kusitishwa mara moja”, “kujiondoa kwa makundi yote ya kigeni” na haja ya “mazungumzo kati ya pande zote”.

Siku moja baadaye, msemaji wa serikali ya Congo alisema “wanatii” tu makubaliano ya Novemba huko Luanda kumaliza mzozo huu.

Rais Kagame alisikitishwa na kwamba suala la waasi linaendelea “kurudi nyuma kwa takriban miongo mitatu” sasa licha ya Umoja wa Mataifa kuwa na “zaidi ya walinda amani elfu kumi” waliotumwa kushughulikia hilo.

Share This Article:

Related posts

Leave a Comment