ONDOENI MIKONO YENU INCHINI KONGO N AAFRICA PAPA AAMBIA MABEBERU

PAPA FRANCIS KUSHOTO NA RAIS TSHISEKEDI WA CONGO KUUME

PAPA KWENYE ZIARA YAKE INCHINI CONGO TAREHE 31 JANUARI 2023

Muda mfupi baada ya kutua Kinshasa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Papa Francis alitoa hotuba iliyojaa shutuma kali za unyonyaji wa raslima za DRC kwa karne nyingi – sio tu kwa nchi hii, bali pia bara.

Alizungumza juu ya ‘mnaso wa kisiasa unaotoa nafasi kwa “ukoloni wa kiuchumi”, ambao alisema ulikuwa sawa na utumwa .

Katika sehemu ya hotuba hiyo iliyopokelewa vyema zaidi aliiambia dunia kutambua maafa ambayo yamefanyika nchini humo na kuheshimu kikamilifu watu wa hapa.

“Iacheni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo! Toen mikono yenu Afrika! Acheni kuisakama Afrika, sio mgodi wa kuvuliwa au eneo la kuporwa,” Papa Francis alisema na kupiga makofi, akimaanisha rasilimali nyingi ambazo zimeleta mingi ya migogoro na vifo kwa nchihiyo.

Walakini, Papa hakurejelea haswa jukumu lililofanywa na wakoloni Wakatoliki, wakiungwa mkono na maagizo ya kihistoria kutoka Vatikani, na ukatili waliofanya hapa.

Wasiwasi kuhusu uwezo wa Papa kutembea

Alizungumza juu ya ulafi ambao hivi majuzi umedhihirika nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kwa maneno yake, “uliyopakwa almasi yake kwa damu,” akimaanisha karibu watu milioni saba ambao wanakadiriwa kuuawa katika vita hapa katika kipindi cha miaka 30 iliyopita.

Wakati safari hii ilipopangwa kutokea mwaka jana, Papa alikuwa amepanga kutembelea mashariki mwa nchi hii kubwa ambapo ghasia mbaya zaidi zinaendelea, na ambapo mamilioni ya watu wameyakimbia makazi yao.

Lakini aliahirisha hadi sasa kwa sababu ya matatizo ya kiafya yanayohusu uwezo wake kutembea na sasa wasiwasi wa usalama unamaanisha hakutakuwa na safari ya kuelekea mashariki.

Share This Article:

Related posts

Leave a Comment